ECUADOR

Kiongozi wa Ecuador Correa ashinda uchaguzi bna kuahidi kuendelea kulinda Mapinduzi ya Taifa hilo

Kiongozi wa Ecuador Rafael Correa ambaye aendelea kusisistiza mapinduzi ya taifa hilo yanazuiliki kwa namna yoyote na wataendelea kuyasimamia kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha hilo linafanyika.

Kiongozi wa Ecuador Rafael Correa akiwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kuendelea na wadhifa wake
Kiongozi wa Ecuador Rafael Correa akiwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kuendelea na wadhifa wake REUTERS/Gary Granja
Matangazo ya kibiashara

Correa ametoa kauli hiyo akisherehekea ushindi ambao ameupata kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi ambao kimefanyika mwishoni mwa juma hili huku matokeo ya awali yakimpa ushindi.

Correa amejigamba kuibuka na ushindi wa asilimia 33 dhidi ya mpinzani wake Guillermo Lasso aliyeambulia asilimi 23.7 ya kura ambazo zimeshahesabia ambapo zaidiya asilimia 57 ya kura zote zikiwa zimehesabiwa.

Kiongozi huyo wa Ecuador amewaambia wafuasi wake ya kwamba wataendelea kusimama kidete kulijenga taifa hilo dogo ili kuhakikisha linakuwa kubwa na imara na kushindana na mataifa mengine.

Correa amesema hawezi akawa tayari kuangalia nchi hiyo ikikwama kusonga mbele kimaendeleo na badala yake atafanya kila linalowezekana kila mwananchi aweze kunufaika na rasilimali za taifa hilo.

Wagombea hao wawili vinara wataepuka duru la pili la uchaguzi wa urais iwapo mmoja kati yao ataibuka na ushindi za zaidi ya asilimia 50 ya kura zote ambazo zimepigwa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Lasso ambaye alikuwa Waziri wa Fedha katika kipindi cha miaka ya 1990 amekiri kushindwa kwenye kinyang'anyiro hicho huku akiwataka wafuasi wake pia kukubaliana na matokeo hayo.

Lasso amesema anakubalia Rais Rafael Correa kuwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho na amemtakia uongozi mzuri katika kipindi kingine cha kuliongoza taifa hilo huku akimtaka kuimarisha utawala bora.