NIGERIA

Wafanyakazi wakigeni saba watekwanyara nchini Nigeria na watu wenye silaha waliofanya shambulizi Jimboni Bauchi

Watu wenye silaha wamewateka wafanyakazi saba wa kigeni katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria huku pia wakimuua mlinzi mmoja na kutajwa kama moja ya shambulizi baya zaidi kutokea katika eneo hilo.

Ramani ya Nigeria ikionesha Jimbo la Bauchi lililoshuhudia utekwajinyara wa raia saba wa kigeni
Ramani ya Nigeria ikionesha Jimbo la Bauchi lililoshuhudia utekwajinyara wa raia saba wa kigeni
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wenye silaha walishambulia eneo ambali ujenzi unaendelea ambapo walifanikiwa kumuua mlinzi mmoja na kisha kutekeleza utekekaji wa watu hao saba raia wa kigeni na kutokomea kulikojulikana.

Jeshi la Poliis nchini Nigeria limethibitisha kutokea kwa shambulizi lililoambata na utekeaji nyara wa raia hao wa kigeni na kwa sasa msako kabambe unaendelea ili kuwatia nguvuni wale ambao wamehusika.

Raia hao wa kigeni walikuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Setraco ambao wanafanya shughuli zao kwenye Jimbo la Bauchi na kuzua hali ya tafrani na hofu ya usalama katika eneo hilo.

Miongoni mwa wale ambao wametekwa nyara ni pamoja na raia wawili wa Lebanon, mmoja wa Italia na mwingine wa Ugiriki ambayo serikali za nchi zao zimeshathibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Msemaji wa Polisi katika Jimbo la Bauchi Hassan Auyo amesema taarifa walizonazo ni kwamba watu hao saba waliokamatwa ni raia wanne wa Lebanon, mmoja kutoka Italia, mmoja kutoka Uingereza na mwingine wa Ugiriki.

Serikali ya Uingereza kupitia ofisi yake ya Mambo ya Nje imekanusha kutokuwa na taarifa za raia wake kutekwa kwenye tukio hilo la shambulia ambalo limetekelezwa na watu wenye silaha huko Bauchi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki Dimitris Avramopoulos kwenye taarifa yake amesema anafanya mawasiliano na Waziri mwenzie wa Italia kuangalia namna ya kuwakomboa mateka wao.

Lawama zimeanza kuekelezwa kwa Kundi la Waislam wenye Msimamo Mkali la Boko Haram ambalo limekuwa mstari wa mbele kutekeleza mashambulizi ya mara kwa mara katika nchi ya Nigeria.