SYRIA

Rais wa Syria Bashar Al Assad atamba Majeshi yake yatashinda kwenye Vita dhidi ya Wapinzani

Rais wa Syria Bashar Al Assad ametangaza Wanajeshi wake watashinda vita dhidi ya Wapinzani
Rais wa Syria Bashar Al Assad ametangaza Wanajeshi wake watashinda vita dhidi ya Wapinzani

Rais wa Syria Bashar Al Assad amerejea tena kauli yake ya kwamba ana uhakiki vikosi tiifu kwa Utawala wake vitashinda kwenye vita ambayo inaendelea dhidi ya upinzani unaotaka kumng'oa madarakani na kufanya mabadiliko ya kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Assad ametoa kauli hiyo alipofanya mahojiano na gazeti moja la nchini Lebanon ambapo amesema wanajeshi wake watashinda na kisha wataongoza mchakato wa maendelea ya kisiasa na kijeshi.

Kiongozi huyo amesema wanashawishika kwa namna ambavyo mapambano yanavyoendelea watashinda kutokana na nguvu waliyonayo katika kukabiliana na vibaraka ambavyo vimekuwa vinatumia na Mataifa ya Magharibi.

Mahojiano hayo kwenye la Gazeti la As-Safir na Rais Assad yamekuja kipindi hiki ambacho Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa UN kutoa pendekezo la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC kuchunguza makosa yanyaofanyika.

Rais Assad ameendelea kusema wanajeshi wao hawatishwi kwa namna yoyote ile na mashambulizi ya wapinzani ambao wanaungwa mkono na Mataifa ya Magharibi na wao wapo tayari kukabiliana nao hadi washinde.

Kiongozi huyo wa Syria amewataka wananchi kuendelea kuiunga mkono serikali yake kwa sababu itaendelea kupigana kwa ajili ya kuwalinda watu wake wasikumbane na madhira ya wapinzania.

Syria iliyoingia kwenye machafuko mwezi March mwaka 2011 imeshuhudia watu wanaokadiriwa kufikia 70,000 wakipoteza maisha kutokana na mapigano baina ya Jeshi la Serikali na Wapinzani.

Tamko la Rais Assad limekuja kipindi hiki ambacho Umoja wa Ulaya EU ukikataa kuondoa muda wa mwisho wa kuwausia silaha wapinzani nchini Syria na badala yake wamekubaliana kuendelea kuwasaidia Viongozi wa Baraza la Mpito kufikia malengo yao.