Komando wa Ufaransa auawa nchini Mali huku raia saba wa taifa hilo wakitekwa nyara nchini Nigeria
Jeshi la Ufaransa ambalo lipo kwenye operesheni ya Kijeshi Kaskazini mwa Mali limepata pigo kwenye operesheni zake baada ya mwanajeshi wake mmoja ambaye yupo kwenye Kikosi cha Makomandoo Harold Vormezeele kuuawa.
Imechapishwa:
Vormezeele ameuawa kwenye mashambulizi ambayo yalizuka baina ya Jeshi la Ufaransa na Wapiganaji wa Makundi ya Waislam ambayo yamefurushwa kutoka katika eneo la Kaksazini mwa Mali.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ndiye amethibitisha kutokea kwa kifo cha Komando Vormezeele na kueleza majonzi yake kutokana na kumpoteza mwanajeshi huyo aliyejitoleza kwenye operesheni ya kumaliza magaidi.
Hollande amesema licha ya kumpoteza mwanajeshi wao mahiri kwenye uwanja wa mapambano lakini hawatorudi nyuma kwenye vita ya ugaidi ambayo wameianzisha katika eneo la Kaskazini mwa Afrika.
Wizara ya Ulinzi wa Ufaransa kwenye taarifa yake imeeleza licha ya Komando wao Vormezeele kupoteza maisha lakini mashambulizi yaliyofanyika yamesababisha vifo vya wapiganaji 20 wa Makundi ya Kiislam.
Huyu anakuwa mwanajeshi wa pili wa Ufaransa kuuawa nchini Mali tangu nchi hiyo ifanye uvamizi wa kijeshi tarehe 11 mwezi Januari ambapo wa kwanza liuawa siku ya kwanza ambaye ni rubani wa helkopta.
Katika hatua nyingine mateka saba wa Ufaransa ambao wametekwa na watu wasiojulikana kwenye mpaka wa Nigeria wamevushwa mpaka na kupelekwa nchini Cameroon serikali ya Taifa hilo imethibitisha.
Watu hao wa familia moja ambao walikuwa kwenye shughuli za utalii wakiwemo watoto wadogo wanne wanaendelea kushikiliwa na watu haom wasiojulikana walijihami vizuri na silaha madhubuti.
Makundi ya Kiislam yanayopatikana Kaskazini mwa Mali yamenyooshewa kidole cha lawama kwa kuhusika na utekeji nyara huo ikiwa ni sehemu ya kutaka kuzorotesha operesheni inayofanywa na Ufaransa nchini Mali.
Rais Hollande amesema utekwaji nyara huo wa raia saba wa Ufaransa hautawakatisha tamaa kwa namna yoyote kwani wanajua hivyo ni vikwazo vya kawaida ambavyo watakabiliwa navyo.