IRAN

Mataifa ya Magharibi yaitaka Iran kuacha kurutubisha nyuklia kabla ya kufanyika mazungumzo chini ya Shirika la IAEA

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad akikagua kinu cha nyuklia cha Natanz ambacho kinaelezwa kupatiwa zana za kisasa zaidi
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad akikagua kinu cha nyuklia cha Natanz ambacho kinaelezwa kupatiwa zana za kisasa zaidi Reuters

Mataifa yenye Nguvu Duniani yameanza kushusha lawama zake kwa Iran siku chache kabla ya kufanyika kwa mazungumzo juu ya nchi hiyo kuendelea na mpango wake wa kitengeneza nyuklia ikidaiwa imeingiza zana za kisasa zaidi kwenye mtambo wake mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa yenye Nguvu Duniani yamenyoosha kidole cha lawama kwa Tehran baada ya Shirika la nguvu za Atomiki Duniani IAEA kutoa taarifa ikieleza Iran imeingiza zana za kisasa zaidi na kuziweka katika kinu chake kimoja cha kuzalisha nyuklia.

Taarifa ya Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA imeeleza zana hizo mpya na za kisasa zimepelekwa kwenye kinu cha kuzalisha nyuklia cha Natanz ikiwa ni ishara nchi hiyo haina mpango wa kusitisha mpango wake wa kutengeneza nyuklia.

IAEA kwenye taarifa yake imesema zana hizi mpya ni za kisasa zaidi na zitaisaidia Iran kutengeneza silaha za nyuklia ikiwa ni pamoja na mabomu na kuendelea kutishia usalama wa dunia.

Mataifa yenye Nguvu Duniani yamesema hatua hiyo ni hatari zaidi hasa kipindi hiki ambacho Iran inatakiowa kuachana na mpango wa kurutubisha nyuklia licha ya Tehran kusema inafanya hivyo kwa sababu ya kuzalisha nishati ya uhakika kwa wananchi wake.

Taarifa hizi zinakuja kipindi hiki ambacho Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA kwa kushirikiana na mataifa yenye ushawishi mkubwa kwenye masuala ya nyuklia yakiandaa mkutano wa kuendelea kuishawishi Iran kuruhusu waangalizi kujionea kile wanacho kifanya.

Serikali ya Marekani kupitia kwa Msemaji wa Ikulu Jay Carney ameionya Iran kutoendelea na mpango wao wa kutengeneza nyuklia licha ya kwamba wamenunua zana za kisasa zaidi na kuzipeleka kwenye kinu chake cha Natanz.

Serikali ya Uingereza nayo imekiri kuguswa mno na taarifa za IAEA kuhusina na Iran kuendelea kuwekeza zana za kisasa kwenye mpango wake wa kutengeneza nyuklia licha ya kutambua unakwenda kinyume na taratibu za dunia.