MALI-UFARANSA

Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam nchini Mali waanza kutumia mbinu ya mashambulizi ya kujitoa Mhanga huko Kidal

Wafuasi wa Kundi la MNLA wakiwa wamejihami vizuri katika Mji wa Kidal ambao umeanza kukumbwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga
Wafuasi wa Kundi la MNLA wakiwa wamejihami vizuri katika Mji wa Kidal ambao umeanza kukumbwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga REUTERS/Cheick Diouara

Majeshi ya Ufaransa nchini Mali yameenderlea kukumbana na upinzani baada ya Wapiganaji wwenye uhusiano na Mtandao wa Al Qaeda Duniani kutangaza wametekeleza shambulizi la kujitoa mhanga karibu na kambi ya wanajeshi hao.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa Kaskazini mwa Mali kwa kutumia bomu lililotegwa ndani ya gari limesababisha watu wawili kujeruhiwa na kuanza kuonesha mbinu mpya zimeanza kutumiwa na Makundi ya Kiislam.

Mlipuko huo wa bomu la kujitoa mhanga ulitekelezwa mita 500 kutoka katika Kambi ya Jeshi inayotumiwa na Majeshi ya Ufaransa na Chad kwenye Jiji la Kidal lililokuwa ngome ya Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam.

Gavana wa Jiji la Kidal amethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo ambapo dereva aliendesha gari hilo hadi karibu na kambi ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa Ufaransa na Chad na kisha mlipuko mkubwa ulisikika.

Kundi la MUJAO ambalo lilisambaratishwa kwenye operesheni ya kijeshi iliyoongozwa na Majeshi ya Ufaransa limesema hakuna ugumu wowote kwao kuweza kuingia Jijini Kidal na kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga.

Msemaji wa Kundi la MUJAO Abu Walid Sahraoui amesema mashambulizi mengi na milipuko imekuwa ikitokea katika mipaka yao kitu ambacho kinaonesha bado wana nguvu ya kushambulia.

Kundi la MUJAO limejigamba kwa sasa limepeleka wapiganaji zaidi katika Mji wa Gao ili kuendelea kupambana na Majeshi ya Ufaransa yaliyofanya uvamizi na kuyasambaratisha Makundi yaliyokuwa yanashikilia eneo hilo.