SYRIA

Muungano wa upinzani nchini Syria walaani ukimya wa mataifa juu ya mauaji yanayoendelea

Raisi wa Syria,Bashar Al Assad ambaye majeshi yake yanaendeleza mapambano dhidi ya makundi mbalimbali yanayopinga utawala wake nchini humo.
Raisi wa Syria,Bashar Al Assad ambaye majeshi yake yanaendeleza mapambano dhidi ya makundi mbalimbali yanayopinga utawala wake nchini humo. REUTERS/Syrian TV via Reuters TV

Muungano wa Upinzani nchini Syria umelaani ukimya wa mataifa katika kushughulikia suala la kupinga mauaji ya raia nchini humo katika kipindi hiki cha mapambano baina ya makundi hasimu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Tamko hilo limekuja baada ya Muungano wa upinzani kusema kuwa unatarajia kuunda serikali yake itakayoongoza maeneo huru nchini humo na kulaumu ukimya wa mataifa hasa kufuatia mashambulizi makubwa ya alhamisi iliyopita ambapo takribani watu mia moja waliuawa.

Katika ghasia zingine ijumaa waangalizi wanabainisha kuwa zaidi ya watu 12 waliuawa baada ya jengo kuporomoka baada ya shambulizi jijini Aleppo.

Upinzani nchini Syria unatarajiwa kuudhuria katika mkutano wa nchi rafiki za Syria huko Roma nchini Italia ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry anatarajiwa kuhudhuria.