Sudani

Mapigano ya kikabila jimboni Darfur yakwamisha Misaada ya kibinaadam

Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir
Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir

Umoja wa Mataifa umeeleza kusikitishwa kwake na Mapigano ya kikabila yanayofanyika katika Jimbo la Darfur nchini Sudan, mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kukimbia mapigano.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa mji wa El Sireaf wamesema kuwa wanamgambo wa kiarabu wametumia Roketi, Maguruneti na Bunduki,wakichoma moto nyumba na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 siku ya jumamosi.
 

Takriban watu 100,000 wamekimbia makazi yao, hatua inayoelezwa kuwa imefanya Operesheni ya kutoa misaada ya kibinaadam kuwa ngumu.
 

Mapigano yalizuka kati ya watu wa jamii ya Rezeigat na mahasimu wao kutoka jamii ya Beni Hussein, mapigano yaliyotokea katika mgodi wa Jebel Amir kaskazini mwa jimbo la Darfur, mwanzaoni mwa mwezi wa Januari.
 

Maafisa nchini humo wamethibitisha kuwa Shambulio hilo limetekelezwa na Watu wa jamii ya Rezeigat ambao wanatoka katika eneo la Magharibu na katikati ya jimbo la Darfur.
 

Machafuko ya sasa nchini Sudan yanaonesha sura mpya ya mzozo wa Darfur, ambapo miaka kumi iliyopita waasi kutoka katika makabila ya watu weusi walianza mapambano dhidi ya utawala uliokuwa na jamii ya kiarabu mjini Khartoum.