Syria

Wanadiplomasia wa Urusi na Syria wanakutana ili kujadili mustakabali wa Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid al-Mualem anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov hii leo wakati Urusi ikitoa shinikizo kwa Upinzani na utawala wa Syria kusitisha mapigano.

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Matangazo ya kibiashara

Juma lililopita Lavrov alisema kuwa kumekuwepo na mwitikio chanya kutoka pande zote mbili wakiwa na nia ya kufanya mazungumzo.
 

Lavrov alisema juma lililopita hakuna suluhisho la kijeshi kutatua mgogoro huo na kua suluhu ya kijeshi ingeleta madhara makubwa zaidi.
 

Umoja wa mataifa umesema Mapigano ya nchini Syria yaliosababisha Watu 70,000 kupoteza maisha tangu kuanza kwa mzozo nchini humo mwaka 2011 yameongezeka siku za hivi karibuni.
 

Taarifa zinasema pamoja na kuwepo kwa jitihada za kumaliza mzozo wa Syria, Waasi nchini humo wamejiondoa katika mazungumzo na Mataifa ya kigeni kwa kile walichodai kuwa Jumuia ya kimataifa imeshindwa kukomesha vitendo vya umwagaji damu.