Kazakhstani

Mataifa yenye nguvu duniani yapunguza makali ya vikwazo kwa Iran

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad
Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad REUTERS/Asmaa Waguih

Mataifa yenye nguvu duniani yamepunguza makali ya Vikwazo kwa Taifa la Iran katika mazungumzo juu ya mpango wa Nuklia wa nchi hiyo, mazungumzo yanayofanyika nchini Kazakhstani.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa Siku mbili mjini Almaty umekuja wakati huu ambapo Vikwazo vimekuwa vikiiweka Iran katika hali mbaya ya kiuchumi.
 

Mataifa yenye nguvu duniani yatatoa ruhusa kwa Iran kuanzisha tena biashara ya dhahabu na vito pia biashara ya kibenki kimataifa ambazo zilikuwa zimewekewa vikwazo.
 

Lakini hatua hiyo imewekewa masharti kwa Iran ambayo ni pamoja kupunguza uzalishaji wa Madini ya Uranium ambayo mataifa hayo yanahofu kuwa yatawezesha kutengeneza Bomu la Nuklia.
 

Mazungumzo haya ya sasa yameelezwa kuleta matumaini tofauti na yale yaliyofanyika Mjini Moscow mwezi June mwaka 2012 ambayo suluhu halikupatikana.
 

Msemaji wa Mkuu wa Sera za mambo ya nje wa umoja wa Ulaya Michael Mann amesema kuwa wamejiandaa kufanya mazungumzo ambayo wanaamini yatanufaisha pande zote mbili.