Kenya

Wagombea urais nchini Kenya washiriki kwenye Mdahalo wa mwisho kuelekea uchaguzi mkuu wa Juma lijalo

Wagombea wanane wa urais nchini Kenya walishiriki jana usiku katika mdahalo wa mwisho kabla ya uchaguzi tarehe 4 mwezi ujao.

Wagombea wa urais nchini Kenya wakichuana katika Mjadala wa jana usiku
Wagombea wa urais nchini Kenya wakichuana katika Mjadala wa jana usiku Reuters
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa maswala nyeti yaliyojadiliwa katika mdahalo huo ni pamoja na maswala ya ardhi ,ufisadi na uchumi.
 

Uhuru Kenyatta anayewania urais kupitia Muungano wa Jubilee alikuwa na wakati mgumu kueleza kiasi cha ardhi anachomiliki yeye na familia yake katika mkoa wa Pwani na maeneo mengine nchini humo na kujitetea kuwa hakuna ushahidi unaomhusisha kuwa alinyakaua au kuiba aradhi ya umma.
 

Kuhusu suala la wakimbizi ambao bado wanaishi katika makambi kutokana na machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007,Uhuru na Odinga walitofautiana hadharani kuhusu kuwapa ardhi watu hao huku waziri Mkuu akisema hakukuwa na fedha kuwapa watu hao .