Ufaransa

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akutana na Rais wa Ufaransa kuzungumzia mzozo wa Mali

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amekutana na Rais wa Ufaransa, Francois Hollande jijini Paris nchini Ufaransa kujadili Mzozo wa Mali.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry
Rais wa Ufaransa Francois Hollande na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Kerry ambaye amesifu mafanikio ya Ufaransa katika Operesheni ya Mali, pia atafanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Laurent Fabius.
 

Operesheni ya Majeshi ya Ufaransa imewafurusha waasi wa makundi ya kiislamu kutoka katika miji mbalimbali kaskazini na Magharibi nwa Mali, hata hivyo Mashambulizi yamekuwa yakiendelea nchini humo.
 

Operesheni ya Mali imekua kiashiria cha mapambano dhidi ya ugaidi baada ya Afghanistan na Washington kupeleka ndege zao za kijeshi kusaidia Majeshi ya Ufaransa nchini Mali, ambayo kwa sasa yanasaidiwa na Vikosi vya Afrika AFISMA.