Kazakhstani

Iran na Mataifa yenye nguvu duniani yakubaliana kukutana tena Mwezi Aprili

Kiongozi wa Ujumbe wa Iran kwenye Mazungumzo ya Nuklia Saeed Jalili
Kiongozi wa Ujumbe wa Iran kwenye Mazungumzo ya Nuklia Saeed Jalili Reuters / Zhumatov

Iran na mataifa yenye nguvu duniani wamemaliza Mazungumzo ya siku mbili hapo jana nchini Kazakhstani na kukubaliana kufanya mazungumzo mengine majuma kadhaa yajayo mazungumzo yatakayolenga Mradi wa nuklia wa Iran.

Matangazo ya kibiashara

Iran imekana shutma kuwa imekuwa ikirutubisha madini ya Uranium kwa kiasi kikubwa na kwa kasi kubwa ili kutengeneza Silaha za Nuklia, shutma ambazo zimekuwa zikitolewa hasa na Israel na Mshirika wake mkubwa, Marekani.
 

Awali suala hili lilijadiliwa katika Mazungumzo kwa awamu tatu katika kipindi cha mwaka mmoja pekee, huku Mkutano wa mwisho uliofanyika mwezi June ulimalizika bila kukubaliana kukutana tena.
 

Mkutano huu pia ulionesha kupiga hatua baada ya Mataifa hayo kupunguza makali ya Vikwazo kwa dhidi ya Iran hasa vya biashara ambavyo vilikuwa vikiiathiri Iran kiuchumi, huku ikiitaka Iran kutazama upya Mradi wake wa urutubishaji wa Madini ya uranium.
 

Iran imesema itakutana tena na  Mataifa hayo  nchini Kazakhstani Tarehe 5-6 Mwezi Aprili.