Uholanzi

Rais wa zamani wa Cote d Ivoire atoa utetezi wake katika mahakama ya ICC kuwa alikuwa akipigania Demokrasia nchini mwake

Rais wa zamani wa Cote d Ivoire, Laurent Gbagbo ameiambia Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC kuwa siku zote amekuwa akiunga mkono Damokrasia nchini mwake.

Kiongozi wa zamani wa Cote d ivoire, Laurent Gbagbo
Kiongozi wa zamani wa Cote d ivoire, Laurent Gbagbo Reuters / Kooren
Matangazo ya kibiashara

Gbagbo ameiambia mahakama ambayo huenda ikamfungulia mashtaka au la Kiongozi huyo wa zamani kutokana na makosa ya uhalifu wa kivita iwapo itajiridhisha.

Gbagbo,67 ni Kiongozi wa kwanza wa zamani kufikishwa katika Mahakama ya kimataifa ambapo anashutumiwa kufanya kampeni kuchochea machafuko wakati wa Uchaguzi wa nchini Cote d Ivoire.

Gbagbo anakabiliwa na Makosa manne ya uhalifu dhidi ya ubinaadam wakati na kuzuka kwa Machafuki makubwa alipokaidi kuondoka madarakani na kumpisha Mshindi wa uchaguzi huo, Allasane Ouattara baada ya kuwepo madarakani kwa kipindi cha miaka 10.
 

Kati ya tarehe 28 mwezi November 2010 na Tarehe 8 mwezi May mwaka 2011, Vikosi vya Gbagbo viliua takriban watu 1000 na kuwabaka Wanawake zaidi ya 35.