Venezuela

Mrithi wa Chavez wa Venezuela kupatikana baada ya uchaguzi wa 14 April

Tume ya uchaguzi nchini Venezuela imearifu kuwa uchaguzi wa raisi atakaye ziba pengo lililoachwa na aliyekuwa raisi wa nchi hiyo Hugo Chavez ambaye alifariki dunia hivi karibuni utafanyika tarehe 14 mwezi April na kuandaa mazingira ya harakati za kampeni.

Henrique Capriles Radonski ameteuliwa tena na muungano wa upinzani nchini Venezuela kuwania kiti cha uraisi.
Henrique Capriles Radonski ameteuliwa tena na muungano wa upinzani nchini Venezuela kuwania kiti cha uraisi. AFP PHOTO/Leo RAMIREZ
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo imetaja tarehe hiyo siku moja baada ya makamo wa raisi Nicolas Maduro kuapa kuwa raisi kivuli katika kipindi ambacho bado raisi hajachaguliwa.

Hata hivyo kulikuwa na maandamano ya kupinga kiapo cha Maduro kwa madai kuwa ni kinyume cha katiba.

Muda mfupi baada ya tarehe kupangwa, muungano mkuu wa upinzani ulimtangaza Henrique Capriles kushiriki kinyanganyiro hicho nafasi ambayo alipoteza kwa Chavez katika uchaguzi wa Oktoba.
 

Uchaguzi huo unakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa raisi wa nchi hiyo Hugo Chavez ambaye alikuwa akiugua na kutibiwa katika hospitali ya kijeshi huko Carcas.