INDIA

Mtuhumiwa wa ubakaji nchini India ajiua gerezani

Mmoja wa washukiwa wanaotuhumiwa kumbaka hadi kufa binti mwenye umri wa miaka 23 nchini India mwishoni mwa mwaka uliopita amejiua kwa kujinyonga wakati akiwa gerezani. Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mshukiwa huyo kwa jina Ram Singh alijinyonga usiku wa kuamkia leo jumatatu akiwa katika gereza la Tihay mjini New Delhi.

Matangazo ya kibiashara

Ram Singh ni mmoja wa washukiwa tano waliokuwa wanashikiliwa na kutuhumiwa kutekeleza ubakaji huo tuhuma ambazo wameendelea kukanusha.

Washukiwa wanaosalia wanatuhumiwa na makosa 13. Ubakaji, mauaji na utekeji nyara ni miongoni mwa makosa mengine waliyoyatenda dhidi ya mwanafunzi huyo wa udaktari aliyekuwa na umri wa miakaa 23.

Tukio hilo la ubakaji lilisabisha maandamano makubwa nchiini India na hata kulaaniwa kimataifa.

Matukio ya ubakaji nchini India yamekuwa yakiongezeka katika siku za hivi karibuni.