Chile-Umoja wa mataifa

Bachelet atangaza kuvua wadhifa wake katika Umoja wa mataifa UN na kurejea nchini Chile

 Michelle Bachelet ametangaza kuacha wadhifa wake kama mkuu wa shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa UN huku kukiwa na uvumi kwamba anatarajia kusimama katika muhula mpya wa uraisi wa Chile katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Mkuu wa masuala ya wanawake katika umoja wa mataifa UN  Michelle Bachelet atangaza kuachia wadhifa huo na kurejea nchini mwake.
Mkuu wa masuala ya wanawake katika umoja wa mataifa UN Michelle Bachelet atangaza kuachia wadhifa huo na kurejea nchini mwake. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bachelet alikuwa kiongozi wa masuala ya wanawake katika umoja wa mataifa UN idara ambayo iliundwa mnamo mwaka 2010 ambapo kabla ya kupewa wadhifa huo alikuwa raisi nchini mwake tangu mwaka 2006-2010.

Bachelet ametangaza kujiondoa kwake katika wadhifa huo ndani ya umoja wa mataifa mwishoni mwa mkutano wa majuma mawili uliojadili hadhi ya wanawake ambapo aliwaambia wajumbe wa mkutano kuwa anarejea nchini mwake.

Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amemsifu mwanamama Bachelet kwa juhudi zake kuziunganisha pamoja idara kadhaa za umoja wa mataifa kwenye masuala ya wanawake na kuwa shirika makini.