EU waitaka serikali ya Cyprus kuachana na mpango wake wa kutoza riba kwa raia wake
Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya EU wameitaka serikali ya Cyprus kuachana na mpango wake wa kutoa riba kutoka kwenye akaunti za wananchi kwenye Benki nchini humo kama njia ya kuhakikisha inapatiwa mkopo wa Euro bilioni kumi.
Imechapishwa:
Mwishoni mwa juma lililopita, serikali ya Cyprus ilitangaza kutoza kodi kwa riba kwa kila mwananchi aliyehifadhi fedha zake benki kama njia moja wapo ya kukabiliana na mdororo wa kiuchumi na kutekeleza matakwa ya Umoja wa Ulaya hatua ambayo ilifanya wananchi wengi kutoa fedha zao benki.
Mawaziri hao badala yake wametaka serikali kutoza kuwango hicho cha riba kwa watu ambao ni matajiri na kuwaacha wananchi wa kipato cha chini ambao wanachini kiwango cha Euro laki moja kwenye akaunti zao.
Rais wa nchi hiyo Nicos Anastasiades amesema kuwa, anafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kupunguza kiwango cha wateja wa Benki nchini humo kuchangia katika mpango huo ili kuzuia maandamnao nchini humo.
Serikali ya Urusi nayo imesema pendekezo hilo la serikali ya Cyrprus kwa wananchi wake si kitu kizuri na pia ni hatari kwa uchumi wa taifa hilo.
Ikiwa pendekezo hilo litaungwa mkono na wabunge watakaopiga kura siku ya Jumanne Benki zote nchini humo zitafungwa ili kuwazuia raia nchini humo kutoa fedha kwenye akaunti zao.