ISRAELI-PALESTINA-GAZA

Rais Barrack Obama aanza ziara ya siku tatu nchini Israel

Rais wa Marekani Barrack Obama anazuru Israel kwa ziara ya siku tatu kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na rais Mamlaka ya Palestina Mohamud Abbas huku usalama ukiimarishwa.

Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa mamlaka ya Palestina wamemtaka rais wa Marekani, Barack Obama anayeelekea kwenye hilo kwa ziara ya kikazi ahakikishe safari hii anakuja na mpango madhubuti wa kumaliza mzozo uliopo kati ya nchi hiyo na majirani zao Israel.

Ziara ya Obama inakuwa ni ziara yake ya kwanza kwenye eneo la Mashariki ya kati toka ateuliwe kwa muhula wa pili ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuzishawishi pande hizo mbili kukubaliana na mpango wake wa kutafuta suluhu mashariki ya kati.

Hivi karibuni serikali ya Marekani ilionesha kutoridhishwa na hatua ambazo zimefikiwa mpaka sasa kati ya Israel na Palestina katika kusaka suluhu ya eneo la ukanda wa Gaza, na hivyo Ajenda kuu ya rais Obama inatarajiwa kusisitiza amani kwenye eneo hilo.

Baadhi ya mataifa ya kiarabu yameikosoa Marekani kwa jinsi inavyoshughulikia mzozo wa Mashariki ya Kati wakidai kuwa yenyewe pekee imechangia kwa sehemu kubwa kutopatikana kwa amani kwenye eneo hilo.

Rais Obama ameedelea kusisitiza kuwa Marekani inaunga mkono juhudi za upatikanaji wa amani na suluhu la kuwepo kwa  taifa la Israel na Plaestina.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas amesema kuwa itasaidia kuishawishi Israel kusaidia kuwaondoa wafungwa zaidi ya elfu moja walioko nchini Israel.