Cyprus

Viongozi wa kisiasa nchini Cyprus wakutana kwa dharura kujadili hali ya kiuchumi nchini humo

Vongozi wa kisiasa nchini Cyprus wanakutana katika kikao cha dharura baada ya bunge kupinga kwa kauli moja mpango wa Umoja wa Ulaya wa kubana matumizi ya fedha nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kinaongozwa rais Nicos Anastasiades kujaribu kutafuta mbinu nyingine ya kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi baada wa wabunge nchini humo kupinga mpango wa awali wa kuwatoza riba  raia wa nchi hiyo.

Naye Waziri wa fedha Michalis Sarris yupo mjini Moscow kujaribu kupata mbinu za kuisadia nchi yake kutoka kwa Urusi ambayo imewekeza katika miradi kutumia Mabilioni za dola.

Ujerumani kwa upande wake inasema ikiwa suluhu halipatikana nchini Cyprus huenda benki nchini humo zisifunguliwe kama kawaida.

Mwishoni mwa juma lililopita,serikali ya Cyprus ilitangaza kutoza kodi kwa riba kwa kila mwananchi aliyehifadhi fedha zake benki kama njia moja wapo ya kukabiliana na mdororo wa kiuchumi na kutekeleza matakwa ya Umoja wa Ulaya hatua ambayo ilifanya wananchi wengi kutoa fedha zao benki.

Mawaziri hao badala yake wametaka serikali kutoza kuwango hicho cha riba kwa watu ambao ni matajiri na kuwaacha wananchi wa kipato cha chini ambao wanachini kiwango cha Euro laki moja kwenye akaunti zao.

Rais Anastasiades amesema kuwa, anafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kupunguza kiwango cha wateja wa Benki nchini humo kuchangia katika mpango huo ili kuzuia maandamnao nchini humo.