KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yatishia kuzishambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Japan

Korea Kaskazini imeonya kuzishambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Japan kitisho kinachozua hali ya wasiwasi katika eneo hilo baada ya Pyongyang kushukiwa kuwa nyuma ya mashambulizi ya mitambo ya utangazaji na Benki za Korea Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi inashuhudiwa katika eneo hilo huku serikali ya Pyongyang ikiendelea kutishia kutumia silaha za Nyuklia kuzishambulia kambi hizo za kijeshi za Marekani nchini Japan na Korea Kusini.

Jeshi la Korea Kaskazini limeonya Marekani kuwa kambi zao nchini Korea Kusini na Japan zitashambuliwa kwa urahisi kutokana na zana zake kuwa na uwezo wa kufika katika maeneo hayo.

Miezi kadhaa iliyopita, Korea Kaskazini ilifaulu kujaribu silaha zake za Nyuklia kuelekea Pwani Magharibi mwa Marekani takriban maili elfu 2 majaribio ambayo Marekani imeonya Korea Kaskazini kuwa ikiendelea na majaribio yake ya silaha itaishambulia

Pyongyang imeendelea kufanya majaribio yake baada ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo zaidi kulizuia kuendelea na mpango huko.

Wiki kadhaa zilizopita, serikali ya Marekani na Korea Kusini zilianza mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwa lengo la kupambana na Korea Kaskazini ikiwa itaivamia Seoul, Tokyo na mataifa ya jirani kwa silaha za Nyuklia.