ICC-MAREKANI-RWANDA

Rais Kagame asema serikali yake inatoa ushirikiano Ntaganda asafirishwe Hague

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema serikali yake inatoa ushirikiano unaohitajika kuhakikisha kuwa kiongozi wa makundi ya uasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo Bosco Ntaganda aliyejisalimisha kwenye Ubalozi wa Marekani nchini humo mapema juma hili anasafirishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Rais Kagame ameongeza kuwa serikali yake inashirikiana na Ubalozi wa Marekani kufanikisha juhudi hizo.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiituhumu serikali ya Kigali kuendelea kuwasaidia waasi wa M 23 Mashariki mwa DR Congo tuhma ambazo serikali ya Rwanda imeendelea kukanusha.

Johnnie Carson Waziri wa Marekani anayehusika na maswala ya Afrika amesema
licha ya changamoto zilizoko mbele yao wana matumaini kuwa watafikia muafaka na serikali ya Rwanda kuhusu kumsafirisha Ntaganda hadi  Hague.

Carson ameongeza kuwa kwa sasa maafisa wa Mahakama ya ICC tayari  wanaelekea Kigali kumsafisha Ntanganda hadi Hague baada ya kujisalimisha katika ubalozi wao mapema juma hili.

Naye kiongozi wa Mashtaka katika Mahakama hiyo Fatou Bensouda amesema Ntaganda atafikishwa katika Mahakama hiyo hivi karibuni kufunguliwa mashtaka yanayomkabili.

 Ntaganda anatuhumiwa kuongoza makundi kadhaa ya uasi Mashariki mwa nchi hiyo kabla ya kupewa cheo katika jeshi la serikali kaa njiamojawapo ya kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.

Aidha, ametuhumiwa kuongoza kundi la waasi la M 23 kulipa silaha ili kukabiliana na serikali ya Kinsasha huku akitihumiwa na Mahakama ya ICC kutekeleza visa vya ukiuwkaji wa haki za bindamu ikiwemo kuwaajiri watoto wadogo katika jeshi lake na pia kutekeleza mauji na ubakaji wa wanawake.

Mahakama hiyo ya ICC imeongeza kuwa kujisalimisha kwa Ntaganda ni habari njema kwa raia wote wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wameteseka mikononi mwa kiongozi huyo wa kundi la waasi.