MALI-UFARANSA

Operesheni ya Jeshi la Ufaransa ikisaidiwa na Wanajeshi wa Ufaransa imefanikiwa kuwasambaratisha Wapiganaji wa Kiislam huko Timbuktu

Wanajeshi wa Mali wakiwa kwenye operesheni ya kuwamaliza Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam katika Mji wa Timbuktu
Wanajeshi wa Mali wakiwa kwenye operesheni ya kuwamaliza Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam katika Mji wa Timbuktu

Majeshi ya Mali yamefanikiwa kuwasambaratisha Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam yanayopatikana katika Mji wa Timbuktu baada ya kuendesha operesheni kabambe mwishoni mwa juma.

Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ilipata msaada kutoka kwa Majeshi ya Ufaransa yaliyo Kaskazini mwa Mali kukabiliana na Makundi ya Kiislam yaliyoshika hatamu kwa kipindi cha miezi tisa tangu kuangushwa kwa Utawala wa Rais Amadou Toumani Toure.

Watu saba walipoteza maisha kwenye mashambulizi baina ya Jeshi la Mali na Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam yaliyoanza siku ya jumamosi baada ya Wanajeshi wa Bamako kuonesha kuchoshwa kwa matukio ya Wapiganaji hao.

Wanajeshi wa Jeshi la Mali wameamua kuchukua hatua ya kuanza kutekeleza operehseni hiyo ya kuwaska wapiganaji wa Makundi ya Kiislam huko Timbuktu kutokana na uwepo wa matukio ya kujitoa mhanga katika siku za hivi karibuni.

Jeshi la Ufaransa lililazimika kutumia ndege za kijeshi kwenye operesheni hiyo kwa kile ambacho kinatajwa nguvu kubwa ambayo walikuwa nayo Wapiganaji hao wa Kiislam kuwazidi wanajeshi wa Mali.

Ufaransa ilishiriki baada ya mwanajeshi mmoja wa mali kupoteza maisha, raia mmoja kuuawa pamoja na wapiganaji wanne wa Makundi ya Kiislam nao wakifikwa na mauti kwenye mapigano hayo.

Duru za Kijeshi huko Bamako zimeeleza kuwa wanajeshi wao wamefanikiwa kuwasambaratisha Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam huku wakiendelea kufanya msako kuangalia kama kuna wale ambao wamesalia.

Maofisa wa Jeshi la Mali wamesema hakuna taarifa za uwepo wa majibishano ya risasi baina ya pande hizo mbili kitu ambacho kinaleta tumaini huenda Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam wamekimbia huko Timbuktu.

Makundi ya Kiislam yalianza mkakati wao wa kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga siku ya jumamosi kitu ambacho kilizusha hofu ya usalama na Jeshi la Mali likaamua kuja na operehseni ya kuwasambaratisha kutoka Timbuktu.