KOREA KASKAZINI

Serikali ya Korea Kaskazini imefungua upya Mtambo wake wa Nyuklia uliofungwa mwaka 2007

Mtambo wa kuzalisha nyuklia wa Yongbyon ambao ulifungwa mwaka 2007 na unatarajiwa kufunguliwa upya
Mtambo wa kuzalisha nyuklia wa Yongbyon ambao ulifungwa mwaka 2007 na unatarajiwa kufunguliwa upya

Serikali ya Korea Kaskazini inayoongozwa na Kim Jong-Un imesema dhamira yake ni kuanza upya kutumia mtambo wake wa kuzalisha nyuklia walioufungwa mwaka 2007 huku pia wakisema huenda wakaanza kuutumia kurutubisha uranium na kutengeza silaha za nyuklia. Serikali ya Pyongyang imetangaza mpango wake wa kufungua upya mtambo wake wa kuzalisha nyuklia kipindi hiki ambacho uhusiano wao na majirani zao wa Korea Kusini ukiendelea kudorora.

Matangazo ya kibiashara

Kitengo cha Nguvu za Nyuklia nchini Korea Kaskazini ndiyo zimetoa tangazo hilo na kusema wameona kuna umuhimu wa kuongeza mkakati wake wa uzalishaji wa silaha za nyuklia ili kujiimarisha kijeshi dhidi ya maadui zao.

Mtambo huo wa kuzalisha nyuklia upo katika eneo la Yongbyon ambapo kulikuwa kunatumika kuzalisha umeme kwa megawati tano pamoja na kuendesha mpango wa kurutubisha uranium.

Kitengo cha Nguvu za Nyuklia kimesema licha ya kuwa na mkakati wa kuanza kurutubisha madini ya uranium lakini pia watatumia mtambo huo kwa ajili ya kuzalisha umeme kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na upungufu wa umeme.

Mtambo huo wa kuzalisha nyuklia unatajwa utasaidia pia maendeleo ya kijeshi katika nchi hiyo inayoendelea kujijenga kijeshi kila kukicha hatua ambayo imekuwa ikiangaliwa kwa jicho tofauti na majirani zake huko katika eneo la Peninsula.

Korea Kaskazini imefungua mtambo huu na kuonekana ni kama jibu la vitendo vya jirani zao wa Korea Kusini ambao kupitia Rais wao Park Geun-Hye ilitangaza haitishwi kwa lolote kutoka kwa jirani zao ambao wametangaza wapo vitani.