SYRIA-UMOJA WA MATAIFA

Umoja wa Mataifa UN umeanza mkakati wa kuhakikisha Syria inaendelea kuwa na mustakabali mwema baada ya kuanguka kwa Rais Assad

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Jan Eliasson aliyetengeza mpango wa maandalizi wa kuisaidia Syria baada ya kuangushwa Rais Bashar Al Assad
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Jan Eliasson aliyetengeza mpango wa maandalizi wa kuisaidia Syria baada ya kuangushwa Rais Bashar Al Assad

Umoja wa Mataifa UN umeanza maandalizi ya kuandaa vikosi vya kulinda amani nchini Syria ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuangushwa kwa serikali ya Rais Bashar Al Assad na nchi hiyo kushikwa na Muungano wa Upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa UN kwenye mapngo wake huo pia wamesema watafanya kila linalowezekana kuhakikisha huduma za kibinadamu nazo zinapatikana kama ambavyo inapaswa licha ya serikali ya Rais Assad kuangushwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Jan Eliasson amesema wamekuwa na mkakati wa chini chini kuangalia namna ambavyo Syria itakuwa baada ya kuangushwa kwa Utawala wa Rais Assad.

Eliasson amesema wamekuwa wakipata uungwaji mkono kutoka mataifa mbalimbali ambayo yameonesha utayari wake kusaidia kuijenga upya Syria punde tu baada ya serikali iliyopo madarakani kuangushwa.

Kauli hii imezua maswali mengi na kuonesha dalili ya kwamba huenda kumekuwa na mpango wa hali ya juu kuhakikisha Muungano wa Upinzani unaingia madarakani na kuiangusha serikali ya Rais Assad.

Mipango huyo ya Umoja wa Mataifa UN imekuwa ikifanywa kwa usiri kwa muda mrefu lakini sasa Naibu Katibu Mkuu Eliasson ameamua kuweka bayana na kusema hawatawaweka kando wananchi na kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu.

Tamko hili linakuja kipindi hiki ambacho takwimu za mauji katika mwezi machi zikitolewa na kuonesha kulikuwa na mauji zaidi ambapo watu wanaokadiriwa kufikia elfu sita na tano wamepoteza maisha.

Shirika la Waangalizi wa Haki za Binadamu lenye makao yake nchini Uingereza katika Jiji la London ndilo limetoa ripoti hiyo ikionesha raia wa kawaida waliopoteza maisha ni elfu mbili na themanini wakiwa watoto mia mbili tisini na nane na wanawake mia mbili tisini na mmoja.

Mkurigenzi wa Shirika hilo la Waangalizi wa Haki za Binadamu Rami Abdel Rahman amesema hali ilikuwa mbaya sana ambapo wapiganaji wa waasi elfu mbili na sabini na wanne nao walipoteza maisha.

Jeshi la Serikali nalo lililopoteza wanajeshi wake elfu moja na sitini na wanne katika kipindi cha mwezi machi pekee kitu ambacho kinaongeza hofu ya usalama katika nchi hiyo iliyo kwenye vita kwa miezi ishirini na tano.

Tangu kuanza kwa mapigano yaliyoingia mwaka wa tatu nchini Syria jumla ya watu elfu sabini wanatajwa kupoteza maisha kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa UN.