KOREA KASKAZINI-MAREKANI

Korea Kaskazini yatoa ruhusa kwa Jeshi lake kutumia silaha za nyuklia kwenye mashambulizi yake dhidi ya Marekani

Jeshi la Korea Kaskazini likiwa kwenye gwaride maalum na sasa limepewa ruhusa ya kutumia silaha za nyuklia
Jeshi la Korea Kaskazini likiwa kwenye gwaride maalum na sasa limepewa ruhusa ya kutumia silaha za nyuklia Reuters

Serikali ya Korea Kaskazini imetoa onyo kwa mara nyingine kwa Marekani na kuitaka itambue Jeshi la nchi hiyo limeruhusiwa kutumia silaha zake za nyuklia kwenye mashambulizi yake. Jeshi nchini Korea Kaskazini limesema mchakati wa kuanza mashambulizi umekuwa ukienda kwa kasi kubwa na huenda wakati wowote iwe leo au kesho wao wanaweza wakashambulia maslahi za Washington.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Pyongyang na kutangazwa na Shirika la Habari la Umma inaeleza kuwa Jeshi kwa sasa limepewa mamlaka kamili ya kutumia zana zao za nyuklia zile ndogo za kati na hata zile kubwa.

Serikali ya Korea Kaskaziniimefia uamuzi huo ili kukabiliana na kitisho cha aina yoyote kinacholewa na Marekani na rafiki zao Korea Kusini kwa Pyongyang na wao wapo tayari kukabiliana na shambulizi lolote lile.

Onyo hilo la Korea Kusini linatajwa kuzidisha hali ya wasiwasi na kudhihirisha dhamira ya nchi hiyo kutaka kuingia vitani na Marekani pamoja na marafiki zake ambao ni Korea Kusini na Japan.

Marekani ilishatangaza mpango wake wa kuweka zana za kujilinda na makombora katika kambi yake huko Guam kitu ambacho kinaonekana kuikera zaidi Korea Kaskazini inayoamini hiyo ni njia ya kutaka kuishambulia.

Tishio hilo la Korea Kusini kuruhusu Jeshi lake kutumia silaha za nyuklia kuwashambulia maadui zake limeanza kuzua maswali huku wengi wakiamini haitakuwa rahisi kwa Pyongyang kutumia silaha hizo zenye madhara makubwa.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel ameendelea kusisitiza nchi yake haiwezi ikatishwa kwa namna yoyoye ile na Korea Kaskazini ambayo imesema itashambulia kambi zake zilizopo nchini Japan.

Waziri Hagel amesema kitu kikubwa ambacho wanakifanya kwa sasa ni kuimarisha ulinzi kwa wananchi wao ambao wanapatikana huko Guam pamoja na kuwarinda rafiki zao Korea Kusini na Japan.

Korea Kaskazini imekuwa mstari wa mbele kutaka kuzishambulia Marekani na Korea Kusini kutokana na kukerwa na tabia ya mataifa hayo kuendesha mazoezi ya kijeshi wakiamini ni kitisho kwa usalama wao.