SYRIA

Rais wa Syria Bashar Al Assad aikosoa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa maamuzi naye na kusema imepoteza uhalali wake

Rais wa Syria Bashar Al Assad amejitokeza na kukosoa maamuzi ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kumtambua Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Ahmed Mouz Al Khatib
Rais wa Syria Bashar Al Assad amejitokeza na kukosoa maamuzi ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kumtambua Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Ahmed Mouz Al Khatib

Rais wa Syria Bashar Al Assad amejitokeza na kuikosoa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kutokana na kutangaza kutomtambua yeye kama Kiongozi wa damascus na badala yake wanautambua Muungano wa Upinzani unaopambana kuingia madarakani. Assad ameishukia Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kusema ni chombo ambacho kimepoteza uhalali kutokana na kushindwa kuwawakilisha wananchi kutoka nchi za Kiarabu na badala yake inawakilishi Mataifa ya Kiarabu pekee.

Matangazo ya kibiashara

Rais Assad ametoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza tangu Jumuiya ya Nchi za Kiarabu utangaze kumtambua Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Syria Ahmed Moaz Al Khatib kama kiongozi wa nchi kwenye mkutano uliofanyika nchini Qatar.

Kiongozi huyo ambaye serikali yake kwa kipindi cha miezi ishirini na tano anapambana na wapiganaji wa upinzani amesema uhalali wa chombo hicho umepotea kutokana na kushindwa kutekeleza matakwa ya wananchi kutoka Mataifa ya Kiarabu.

Assad amesema uhalali wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu hautokani na uwepo tu wa chombo hicho au sera zao za ndani na nje bali kile ambacho wanakifanya kwa wananchi kutoka nchi wanachama za Jumuiya hiyo.

Rais Assad ameongeza matukio ya hizi karibuni ndiyo yanaonesha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imepoteza uhalali wake kama chombo kinachopaswa kusimamia haki ya usawa wa wananchi kutoka nchi wanachama.

Kauli ya Rais Assad ameitoa alipofanya mazungumzo na gazeti la Aydinlik na Televisheni ya Ulusal zote za nchini Uturuki huku pia akimtuhumu Waziri Mkuu wa Taifa hilo Recep Tayyip Erdogan kutokana na kuwa kigeugeu.

Assad amekiri kushangazwa na hatua ya Waziri Erdogan kushindwa kuwa na msimamo tangu kuanza kwa vita nchini Syria na kudumu kwa kipindi cha miezi ishirini na tano na kuchangia madhara makubwa.

Watu zaidi 70,000 wanatajwa kupoteza maisha nchini Syria tangu kuanza kwa vita hivyo na kusababisha watu wengine 260,000 kukimbilia nchi za jirani kuomba hifadhi ya ukimbizi ikiwa ni Uturuki na Jordan.