JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-CHAD

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ECCAS wakataa kumtambua Michel Djotodia kama Kiongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa Chad Idriss Deby akiongea na Wanahabari na kueleza uamuzi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati kutoutambua Uongozi wa Michel Djotodia
Rais wa Chad Idriss Deby akiongea na Wanahabari na kueleza uamuzi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati kutoutambua Uongozi wa Michel Djotodia Photo AFP / Bertrand Guay

Viongozi kutoka Mataifa Wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ECCAS wamekataa kwa pamoja kuitambua serikali inayoongoza Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kufanyika kwa mapinduzi zaidi ya majuma mawili sasa.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wametoa kauli hiyo kwenye mkutano wao uliofanyika nchini Chad ikiwa na lengo la kujadili hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kuangushwa kwa serikali ya Rais Francois Bozize aliyekimbilia uhamishoni.

Marasi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ECCAS wamesema hawamtambui Michel Djotodia kama Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na kuingia madarakani kwa njia zisizo za kidemokarasia.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati ECCAS imependekeza kuundwa kwa Kamati Malum ambayo ipewe jukumu la kuongoza nchi kwa kipindi cha miezi kumi na minane kabla ya kuitishwa uchaguzi mkuu.

Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Chad Idriss Deby amewaambia wanahabari maazimio yaliyofikiwa ni kutoitambua serikali inayoongozwa na Muungano wa Seleka chini ya Djotodia ana Waziri Mkuu Nicolas Tiangaye.

Rais Deby ameswma ilikuwa vigumu kwa Jumuiya yao kumtambua Rais ambaye amejipa madaraka mwenyewe baada ya kuiangusha serikali iliyokuwepo na ndiyo maana wamependekeza Kamati Maalum iongoze nchi.

Kando ya Mkutano huo Waziri Mkuu Tiangaye akawaambia wanahabari wamepokea mapendekezo yalitotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati na wanahakikisha wanayafanyia kazi.

Naye Waziri Mkuu wa zamani Martin Zigele amesema muda huu si wa kuendelea na malumbano ya kwamba nani anapaswa kuongoza au nani anafaa kuwa Rais badala yake wanapaswa kuawangalia wananchi wa Miji na Vijijini wanavyoteseka.

Zigele amesema wananchi wanakabiliwa na hali ngumu mno kutokana na madhila ya machafuko yaliyoshuhudiwa na haitmaye kuangushwa kwa serikali ya rais Bozize iliyokuwa inatawala.

Muungano wa Seleka chini ya Kiongozi wake Djotodia ulifanikiwa kuchukua madaraka tarehe 24 Machi baada ya kufanikiwa kuingia makazi ya rais ambaye alikimbia na kuomba hifadhi katika nchi za jirani.

Muungano wa Seleka uliamua kuanzisha vita upya dhidi ya jeshi la serikali kutokana na kukerwa na hatua ya kupuuzwa kwa madai yao kulikofanywa na rais Bozize licha ya kufanyika kwa mazungumzo ya zamani huko Libreville nchini Gabon.