INDIA

Watu 29 wapoteza maisha nchini India baada ya Jengo la Ghorofa 7 lililokuwa linajengwa kuanguka

Kikosi cha Uokoaji kikiondoa mabaki ya kifusi cha ghorofa kusaka watu walionaswa chini nchini India
Kikosi cha Uokoaji kikiondoa mabaki ya kifusi cha ghorofa kusaka watu walionaswa chini nchini India

Watu 29 wanatajwa kupoteza maisha nchini India na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa baada ya kuanguka kwa jengo la ghorofa saba lililokuwa linaendelea kujengwa katika Mji wa Mumbai.

Matangazo ya kibiashara

Watu wanaofikia 60 wameokolewa kutoka katika kifusi kilichosababishwa na kuanguka kwa jengo hilo ambapo wengi wa waliopoteza maisha ni wafanyakazi pamoja na familia ambazo zilikuwa zinaishi.

Jengo hilo la ghorofa saba limeanguka na kusababisha kifusi chenye urefu wa mita 8 kitu ambacho kimekuwa kikwazo kwa kikosi cha uokoaji kuwafikia watu wanaotajwa kufukiwa chini.

Kikosi cha Uokoaji kimeendelea kupambana kuhakikisha kinawafikia watu wanaosemakana kufukiwa na kifusi hicho huku zana za kisasa zikikosekana kupatikana kwa wakati na kuchangia zoezi kuwa gumu.

Kamishna wa Polisi katika Wilaya ya Thane K.P. Raghuvanshi amesema waambia wanahabari wameshapata miili ya watu 29 na kuwaokoa wengine 60 huku wengi wao wakiwa wamejeruhiwa.

Raghuvanshi ameweka bayana wengi wa waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni wahamiaji kutoka Mumbai ambao wamekuja kusaka kazi za ujenzi ni kupata malipo ya siku hivyo kuishi hapo wakiwa na wake zao pamoja na watoto.

Serikali ya Mtaa katika eneo hilo imeahidi kufanya uchunguzi wa sababu za kuanguka kwa jengo hilo la ghorofa sambamba na kupitia ubora wa majengo mengine ambao yanapatikana katika Mji huo.

Msemaji wa Manispaa ya Thane Sandeep Malwi amesema jengo hilo lililoanguka halikuwa na kibali cha kujenga na hivyo watafanya uchunguzi kujua ni kwa nini liliendelea kmujengwa na kisha watatoa ripoti yao.

Vyombo vya habari nchini India vimeripoti sababu za kuanguka kwa jengo hilo la ghorofa saba ni udhaifu wa vifaa ambavyo vimetumika vinavyotajwa hazina ubora unaofaa kwa majengo kama hayo.