RWANDA

Rwanda yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 19 ya mauaji ya kimbari

RFI

Wananchi wa Rwanda wameanza rasmi maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka kumi na tisa ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994 na kusababisha takribani watu milioni moja kuuawa katika kipindi cha siku mia moja.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameungana na Wanyarwanda wote na pia amewasha mwenge wa matumaini ambao utawaka kwa muda wa juma zima la maombolezo hayo.

Kumbukumbu hizo zinaambatana na utembeleaji wa makaburi na maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mauaji hayo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa salamu kwa wahanga wa mauaji hayo ya nchini Rwanda na kusema kwamba Umoja wa mataifa UN inachukua hatua kila siku kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena.