SUDAN-UINGEREZA-QATAR

Uingereza yaahidi msaada zaidi ili kuiimarisha serikali ya Sudan

Waziri wa Maendeleo ya kimataifa wa Uingereza, Lynne Featherstone
Waziri wa Maendeleo ya kimataifa wa Uingereza, Lynne Featherstone guardian.co.uk

Uingereza imeahidi pesa za ziada kwa serikali ya Darfur katika miaka mitatu ijayo ikiwa ni jitihada za kusaidia watu wa Sudan kuwa na uwezo wa kujitegemea, ahadi hiyo imetolewa katika mkutano wa wafadhili wa kimataifa ambao wamekutana mjini Doha nchini Qatar mapema jumapili hii.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo serikali ya London imesema itatoa takribani yuro milioni 13 ili kuwezesha jamii za huko Sudan kujiimarisha na kutoa ujuzi kwa watu ili kupata shughuli za kujiingizia kipato.

Takribani wajumbe mia nne wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya msaada na serikali mbalimbali wamekutana kwa lengo la kuisaidia Darfur kurejea katika mkakati endelevu wa kujikwamua kijamii.

Waziri wa maendeleo ya kimataifa Lynne Featherstone kutoka Uingereza alibainisha kuwa mkutano huo unawapa fursa kubwa watu wa Darfur kupata uungwaji mkono wanaohitaji ili kuepuka vita na utegemezi wa misaada ya dharura.