Afghanistani

watu 9 wapoteza maisha na wengine 22 wamejeruhiwa baada ya basi waliokuwemo kukanyaga bomu

Shambulio la basi lilikonyaga bomu la kutegwa ardhini
Shambulio la basi lilikonyaga bomu la kutegwa ardhini

Watu 9 wameuawa na wengine 22 wamejeruhiwa mapema leo asubuhi baada ya bus waliokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la kutegwa ardhini katika mji wa Wardak kusini magharibi mwa Kaboul, mji ambao unakumbwa na misukosuko ya usalama mdogo kwa kipindi kirefu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kiongozi wa mkoa wa Wardak Attaullah Khogyani amesema kwamba tukio hilo limetokea asubuhi ya leo saa nane na kukiri kuwa watu 15 wapo katika hali mbaya na kuwatuhumu wanamgambo wa Taliban kuhusika katika tukio hilo na kuendelea kuwa Talibans pekee ndio wanaojihusisha na vitendo vya kutega bomu za ardhini.

Ghulam Farouk Wardak, mkurugenzi wa afya katika mji wa Wardak amesema kuwa mwanamke mmoja yumo kati ya watu 9 waliouawa pamoja na watoto 3 katika majeruhi.

Mashuhuda wanasema bus hilo lilikuwa limepakia watu wengi, wachache pekee ndio waliohusurika.

Mji wa Wardak Kusini Magharibi mwa mji wa Kaboul ni mji ambao umekosa utulivu kwa kipindi kirefu ambao umekuwa ukitumiwa na wanamgambo wa Talibans ambao wamekuwa wakiendesha mashambulizi ya mara kwa mara.

Hili ni tukio la nne kubwa kutokea nchini Afghanistani katika kipindi cha juma moja wakati yakianzishwa tena mapigano baada ya ukimya wa kipindi kadhaa.

Jumatano juma lililopita Talibans ambao wanasakwa kwa udi na uvumba na jamii ya kimataifa bila mafaanikio, walishambulia mahakama moja magharibi mwa Afghanistani na kuwauwa watu 46.

Jumamosi tukio la kujitowa muhanga dhidi ya ujumbe wa Marekani liligharimu maisha ya wanajeshi watatu na raia wawili wa Marekani Kusini mwa nchi hiyo.

Siku hiyo hiyo mashambulizi ya anga ya ndege za NATO yamewauwa watoto 11, ambapo mashambulizi hayo yamekuja baada ya makabiliano baina ya wanamgambo wa Talibans na majeshi ya Marekani pamoja na yale ya Afghanistani ambapo raia mmoja wa Marekani alipoteza maisha.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ametaka uchunguzi wa kina na wa haraka ufanyike kubaini chanzo cha kutekelezwa shambulizi la angani lililofanywa na Wanajeshi wa Jeshi la NATO na kuchangia vifo vya watoto kumi na mmoja.

Rais Karzai kwenye taarifa yake kuelekea kwa Viongozi wa NATO nchini Afghanistan ametaka kupatiwa maelezo ya kina juu ya kile kilichosababisha watoto hao kushambuliwa na wakiwa kwenye Jimbo la Kunar.

Hili ni shambulizi jingine baya kulenga raia nchini Afghanistan na kuchangia kuzuka kwa hasira kutoka kwa wananchi na hapa Msemaji wa Majeshi yanayolinda amani ya ISAF Richard Spiegel anathibitisha kutokea kwa vifo hivyo.