Uingereza

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher afariki dunia

Margaret Thatcher wakati wa uhai wake
Margaret Thatcher wakati wa uhai wake REUTERS/Luke MacGregor/Files

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher amefariki dunia leo jumanne akiwa na umri wa miaka 87 kutokana na shinikizo la damu linalopelekea kupata mshtuko wa moyo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa iliotolewa na msemaji wa kiongozi huyo wa zamani Lord Tim Bell “ Ni kwa uchungu mkubwa Mark na Carol Tatcher wanatangaza kifo cha mama yao Margaret Tatcher aliefariki leo asubuhi kutokana na mshtuko wa moyo.

Katika taarifa uliotolewa na waziri mkuu wa sasa wa Uingereza David Cameron ambae anatoka chama kimoja na hayati huyo cha kihafidhina amesema wamempoteza kiongozi shupavu, kabla ya kutangaza kusitisha ziara yake barani Ulaya kurejea kuomboleza.

Upande wake Malkia Elizabeth II katika taarifa iliotolewa kutoka Buckingham amesema kusikitisha na kifo cha kiongozi huyo wa zamani na ametuma salam za rambi rambi kwa familia.

Margaret Thatcher ndiye mwanamke pekee ambaye ameshawahi kuwa waziri mkuu nchini Uingereza katika karne hii ya XX, na alikuwa hajaonekana hadharani kwa kipindi cha muda mrefu, tangu mwaka 2002 kufuatia ushauri wa ma dactari na kutokana na kupata mshtuko wa mara kwa mara.