SYRIA-UN

Ban Ki Moon aitaka serikali kutowa ushirikiano kwa tume ya uchunguzi dhidi ya matumizi ya bomu za sumu

Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amewatolea wito viongozi wa Syria kutowa ushirikiano kwa tume ya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wanaotaraji kutumwa huko kuchunguza iwapo bomu za sumu zimetumiwa katika mchafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukutana na viongozi wa Italia pamoja na baba mtakatifu, Francisco Ban ameviambia vyombo vya habari kwamba ameitaka serikali ya Syria kutowa mchango wake wa dhati na kuruhusu ujio wa tume hiyo ya uchunguzi.

Katibu mkuu Ban Ki Moon amekumbusha kwamba tayari amekutana na wajumbe wa serikali ya Syria marchi 20 na wale wa Uingereza na Ufaransa marchi 21 na hadi leo hajapata taarifa yoyote ya serikali ya Syria kuhusu jambo hilo.

Serikali ya Syria na waasi wanatuhumiana kila upande kutumia silaha za sumu katika mapigano jijini Aleppo na Damascus.

Serikali ya Dasmcus ilikuwa imetupilia mbali tume hiyo ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uchunguzi kama ilivyokuwa imependekezwa na katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon ya kutuma wajumbe hao katika maneo yote ya Syria. Kulingana na kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Syria ambae amesema kwamba Ban anatishwa na vitiaho vya mataifa ya magharibi yanayo changia umwagaji wa damu nchini Syria, bila hata hivo kuyataja mataifa hayo.

Waziri huyo amesema serikali ya Damascus imeomba Umoja wa Mataifa kutuma tume ya kiufundi isioegemea upande wowote na yenye busafa katika vijiji vya Khan Aassal mjini Aleppo eneo la akskazini kuchunguza kuhusu yaliojiri katika eneo hilo lililolengwa siku za nyuma na bomu iliokisiwa kuwemo kemikali zenye sumu zilizo tumiwa na makundi ya waasi.

Ban Ki Moon ameendelea kutamka kuwa lengo kubwa hasa la tume hiyo nchini Syria ni tukio la Khan Aassal, lakini kufuatia taarifa alionazo kuna umuhimu wa kuchunguza pia tukio la Homs Desemba 23 mwaka jana.

Baada ya barua ya serikali ya Syria, kutaarifu matumizi ya bomu za somu kwa waaasi, Uingereza na Ufaransa ziliomba Umoja wa Mataifa kuchunguza taarifa hizo