KENYA-KENYATTA

Sherehe za kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta za fana licha ya kutokuwepo marais wa nchi za magharibi

Uhuru Kenyatta wakati wa kula kiapo
Uhuru Kenyatta wakati wa kula kiapo par THOMAS MUKOYA/Reuters

Sherehe za kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta zimefanyika kwa shangwe na nderemo mbele ya marais wa nchi za Afrika, hata hivyo vingozi wa nchi za magharibi hawajahudhuria sherehe hizo kutokana na aibu juu ya mashtaka dhidi ya Bwana Kenyatta na makam wake Willaim Ruto dhidi ya uhalifu wa kibinadamu na ushirika wao katika madai ya unyanyasaji baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Matangazo ya kibiashara

Mbele ya halaiki ya watu Uhuru Kenyatta ameapa akisema kwamba: “Mimi Uhuru Kenyatta, nafahamu uzito wa majukumu yangu kama Rais wa Jamhuri ya Kenya, Naapa uaminifu na utii kwa Jamhuri ya Kenya,"

mkewe Margaret, akishikilia Biblia ambayo aliyowekea mkono kwa kula kiapo kitabu ambacho hicho hicho ndicho alichoshikilia hayati baba yake Jomo Kenyatta wakati wa kuapishwa kwake kama rais wa kwanza mwaka 1964.

Rais mpya pia aliahidi "kulinda na kutetea uhuru, uadilifu na hadhi ya watu wa Kenya," wakati wa sherehe za kuapishwa kwake zilizokuwa chini ya ulinzi mkali.

Uhuru Kenyatta mwenye umri wa miaka 51 anakuwa rais wa kwazna mwenye umri mdogo nchini Kenya na wa kwanza kuchaguliwa licha ya kuwa na keshi ya kujibu kwenye mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC.

Makam wake wa rais William Ruto ambae pia anashtakiwa na mahakama hiyo ya ICC kutoka jamii ya wa Kalenjin alikua kiapo pia kushika hatamu ya uongozi.

Mgeni wa heshima katika sherehe, Rais wa Uganda Yoweri kaguta Museveni amewapongeza wa Kenya kutupilia mbali vitisho na vitimbi vya mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC kwa kumchaguwa Uhuru Kenyatta kuwa rais wa jamuhuri ya nne ya Kenya.

Akizungumza katika sherehe za kuapishwa kwa rais Uhuru Muigaye kenyatta kama Rais na William Samoe Ruto waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu nchini Kenya na ambao wanatakiwa kiripoti katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC Julay 9 baada ya tuhuma za kuhusishwa katika mauaji ya baada ya uchaguzi ya mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya elfu moja walipoteza maisha huku watu kadhaa wakiyatoroka makwao.