IRAN-IRAQ

Ndege za Iran zinazoelekea nchini Syria zafanyiwa msako nchini Iraq

DR

Vyombo vya usalama nchini iraq vimeendesha msako dhidi ya ndege ya Iran iliokuwa ikiruka katika anga zake ikielekea nchini Syria, na kukuta pekee bidhaa mbalimbali za misaada ya kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Hili likiwa ni tukio la pili katika kipindi cha majuma mawili tangu pale serikali ya iraq ilipotangaza hatuwa yake ya kuendesha msako kwa ndege zinazoelekea nchini Syria kama ilivyo agizwa na Marekani. Serikali wa Washington inashuku ndege za Iran zinazo safirisha misaada ya kibinadamu hutumia fursa hiyo pia kwa kupeleka vifaa vya kijeshi lwa utawala rais Bashar al Assad.

Msemaji wa waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki, Ali al- mousaoui amesema vyombo vya usalama nchini Iraq vimepekua ndegbe ya shirika la Iran la Mahan Air, na kukuta pekee midhaa mbalimbali za kibinadamu.

Hapo jana ndege moja ya Iran ilifanyiwa upekuzi katika hali kama hiyo, na baadae kukuta vifaa vya Hospitalini pekee kinyume na ilivyo tarajiwa.

Serikali ya Teheran ilipinga tukio hilo la kwanza kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Ramin Mehmanparast ambae alighadhabishwa na kitendo hicho alichokisema kina taka tu kuleta hofu kwa Iran, chini ya kampeni za Marekani na nchi za magharibi zinazoungana na mataifa hayo aliyo yaita dhalimu.

Msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje amesema kuwa hakika kitendo hicho kilichoendeshwa na Iraq chini ya shinikizo la Marekani ni dalili tosha kwamba hakuna ukweli wowote kuhusu shutma dhidi ya Iran kwamba inapelekea vifaa vya kijeshi nchini Syria.

Katika kipindi cha miezi hii, Utawala wa Obama umekuwa ukiiomba Iraq kuendesha msako dhidi ya ndege zinazoelekea Syria kupitia Iraq.

Katika ziara yake jijini Bagdad Marchi 24 iliopita, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alionya kuwa misafara ya ndege zitokazo Iran kuelekea Syria inachangia kusafirisha silaha kwa utawala wa Bashar al Assad.

Hadi leo serikali ya Iraq ilijizuia kuonyesha msimamo wake kuhusu vita vya nchini Syria vilivyo gharimu maisha ya watu wanaokadiriwa kufikia elfu sabini kwa kipindi cha miaka miwili