JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-OIF

Shirika la kimataifa la nchini zinazo zungumza lugha ya kifaransa lasitisha uanachama kwa serikali ya jamhuri ya Afrika ya kati

Louis Michel mjumbe maalum wa OIF nchini Afrika ya kati
Louis Michel mjumbe maalum wa OIF nchini Afrika ya kati

Shirika la kimataifa la nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa Francophonie(OIF) limetangaza kusitisha kwa muda uanachama wa jamuhuri ya Afrika ya kati kwenye shirika hilo kufuatia mapinduzi ya waasi wa Seleka waliomfurusha madarakani rais Francois Bozize, na kuwataka waasi hao madarakani kutekeleza mapendekezo ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya kati kwa ajili ya taasisi za kipindi cha mpito.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la kudumu la shirika hilo litajadili na kutathimini uamuzi huo katika kikao kitachofanyika Juni 28 mwaka 2013, huku baraza hilo likiwa tayari kuchangia katika mchakato wa uundwaji wa taasisi za kipindi cha mpito zitazo jumuisha pande zote.

Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Ubelgiji Louis Michel ambae ni mjumbe maalum wa OIF nchini Afrika ya kati ambae amerejea hivi karibuni kutoka nchini jamuhuri ya Afrika ya Kati amesema kwamba hatuwa hiyo iliochukuliwa ni ya muda, ili kulazimisha utekelezaji wa mapendekezo ya uundwaji wa taasisi za kipindi cha mpito.

Iwapo viongozi wa kipindi cha mpito kuonyesha nia njema, kama walivyoonyesha, wakitekeleza maamuzi ya viongozi wa CEEAC ya kikao cha jijini N'Djamena ili nasi tujadili na kutathmini hatuwa hii, amefahamisha hayo wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya kati walikutana jijini N'Djamena April 3 mwaka huu na kutowa mapendekezo ya kipindi cha mpito nchini jamuhuri ya Afrika ya kati, yatayo towa fursa ya kuwepo kwa uchaguzi wa rais wa kipndi cha mpito kwa kpindi cha miezi 18 na uundwaji wa baraza la kitaifa la kipindi cha mpito, mahakama ya kikatiba na serikali ya muungano wa kitaifa.

Shirika la OIF linaundwa na mataifa 56 na serikali wanachama. Nchi tatu zimesitishiwa uanachama, ikiwemo jamuhuri ya Afrika ya kati, Mali, Madagscar na Guinea Bisau.
Katibu mkuu wa OIF Abdou Diouf alilaani vikali marchi 25 wakati makundi ya uasi wa Seleka walipoiteka nchi na kumuondowa rais Francois Bozize, ambae waasi hao wa Seleka walimtuhumu kutoheshimu makubaliano ya amani ya jijini Libreville.