Afrika kusini-jamhuri ya Afrika ya kati

Majeshi ya Afrika Kusini yaliokuwa nchini nchini Afrika ya kati yaondoka kujiandaa kuelekea nchini DRCongo

wanajeshi wa Afrika Kusini waliokuwa nchini jamuhuri ya Afrika ya Kati
wanajeshi wa Afrika Kusini waliokuwa nchini jamuhuri ya Afrika ya Kati

Majeshi yote ya Afrika Kusini yaliokuwepo nchini jamuhuri ya Afrika ya kati yamerejeshwa nyumbani wakati huu upinzani ukiendelea kuwa na mashaka kuhusu uhalali wa uwepo wa vikosi hivyo nchini jamuhuri ya Afrika ya kati vilivyotumwa na rais Jacob Zuma nchini humo wakati ikitarajiwa kutuma kikosi kingine nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Afrika kusini Xolane Mabanga amesema wanajeshi wate waliokuwa wametumwa nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati tayari wamerejea nyumbani wakiwa salama ambapo amesema wanajeshi 13 waliuawa huku wengine 27 wakijeruhiwa wakati wa kuanguka kwa jiji la Bangui Marchi 24, hakuna waliopotea, ni jukumu la waasi kusema idadi ya wanajeshi 36 au 50 wameipata wapi, amesisitiza hivo.

Miongoni mwa waliojeruhiwa tisa bado wamelazwa Hospitalini mmoja akiwa katika hali mahtuti, kwa sasa hakuna mwajaeshi mwingien alibaki nchini jamuhuri ya Afrika ya Kati amefahamisha hayo Mabanga.

Jeahi la Afrika kusini limepata pigo kubwa sana nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati tangu kuundwa kwake mwaka 1994.

Tukio hilo linaendelea kuzua mjadala, ambapo kulikuwa na wakufunzi wa kijeshi zaidi ya thalathini mwaka 2007, na zaidi ya wanajeshi mia mbili januari mwaka huu.

Ikulu ya Afrika Kusini imekanusha habari za kuwepo kwa makubaliano baina ya ya rais Jacob Zuma na Francois Bozize, baada ya upinzani kuweka bayana nyaraka za makubaliano kati ya nchi hizi mbili yaliosainiwa mwaka 2006, yaliovuka mbali na ushirikiano wa kijeshi lakini pia ushirikiano kwenye secta ya nishati na madini.

Upinzani unahoji kuhusu faida za Afrika Kusini nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Mvutano huo unajiri wakati jeshi la Afrika Kusini likijiandaa kuelekea nchini jamuhuru ya Kidemokrasia ya Congo kujiunga katika kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa mashariki mwa DRCongo kitacho pambana na makundi ya waasi.

Msemaji wa jeshi la Afrika Kusini Xolane Mabanga amesema wapo tayari kwa safari ya kuelekea mashariki mwa DRCongo kwa sasa wanasubiri kuitwa na Umoja wa Mataifa.