LONDON-SYRIA

Mawaziri wa G8 kukutana na waasi jijini London kabla ya mkutano wa viongozi wa nchi hizo

mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tajiri duniani katika kikao cha April 12 mwaka 2012 jijini Washington
mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tajiri duniani katika kikao cha April 12 mwaka 2012 jijini Washington

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zenye utajiri mkubwa duniani G8 akiwemo wa Marekani John Kerry wanakutana jijini London na waasi wa Syria siku moja kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa nchi hizo tajiri duniani wataojadili kuhusu Syria, Korea Kaskazini, Iran, Myanmar.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa waasi Ghassan Hitto na makam wa rais wa muungano wa waasi wa Syria Georges Sabra na Souheir Atassi ambao wanataraji kuzindua ombi lao la kutaka wapewe silaha, ili waendelee kupambana na wanajeshi wa serikali ya rais Bashar al Assad.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alidokeza jana kwamba swala la Syria litapewa kipao mbele katika mkutano huo wa viongozi wa nchi 8 zenye utajiri mkubwa duniani.

Akiwa jijini Tel aviv, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alifahamisha kwamba atakutana na upinzani wa Syria jijini London na kujadili kuhusu hatuwa mbalimbali za kufikia ufanisi wa kuung'oa utawala wa rais Bashar al Assad.

William Hague alifahamisha kwamba alikuwa na mazungumzo jana na viongozi watatu wa waasiw a Syria na kugusia swala la kuwapa waasi silaha na kuongea kuwa Uingereza na Ufaransa zitaendelea kuunga mkono na kutetea hatuwa ya kuondowa vikwazo vya Umoja wa ulaya dhidi ya kuwapa silaha waasi wa Syria.

Hague amesema kwamba iwapo hali itaendelea kuwa mbaya zaidi ilivyo kwa sasa, swala la kuwapa waasi silaha halitaepukika.

Upande wake John Kerry waziri wa mambo ya nje wa Marekani akiulizwa kuhusu Marekani kuwapa msaada wa kijeshi waasi wa Syria, amesema kuwa hilo ni swala la ikulu ya Marekani ambapo kwa sasa Serikali ya Washington inapinga swala hilo la kutowa silaha kwa waasi kwa hofu ya kuona silaha hizo zinaanguka mikononi mwa magaidi, ambapo amesema anapendekeza njia za kidiplomasia.