NIGERIA-BOKO HARAM

Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria akataa mpango wa msamaha kwa kundi lake

Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram
Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram

Kiongozi wa kundi la kiislamu lenya msimamo mkali Boko Haram nchini Nigeria Abubakar Shekau, amekataa mpango wa kupatiwa msamaha kwa Wanamgambo hao ambao uliahidiwa na Ofisi ya Rais kuwa itatathimini Mpango huo ili kukomesha mauaji nchini humo,

Matangazo ya kibiashara

Abubakar Shekau ndiye Kiongozi wa Kundi la Boko Haram ambaye ametajwa na Marekani kwenye orodha kuwa mmoja wa Magaidi, amedai kuwa kundi lake halijafanya makosa yeyote hata ikapewa mshamaha, badala yake amesema Boko haram inatoa msamaha kwa Serikali ya Nigeria kwa kuwa kinyume na maelekezo ya uislamu.

Juma lililopita, Rais Goodluck Jonathan aliunda jopo la kuangalia uwezekano wa kutoa msamaha kwa Wanamgambo, ambao vitendo vyao vya mashambulizi vimesababisha zaidi ya watu 3,000 kuuawa tangu mwaka 2009, ikiwemo mauaji yaliyotekelezwa Askari wa usalama.

Jopo hilo limeripotiwa kuwa na Maafisa wa usalama, Viongozi wa Kaskazini mwa Nigeria na Wawakilishi wengine,ambapo jopo hilo linatarajiwa kutoa Ripoti yake baadae Mwezi huu.

Serikali ya Nigeria liliahidi kutoa msamaha kwa Wanamgambo katika eneo la jimbo la Niger Delta mwaka 2009,hatua ambayo ilisaidia kuondoa hofu ya kukosekana kwa hali ya usalama katika eneo hilo.