Korea kaskazini-Marekani

Marekani yaionya Korea Kaskazini kuacha kucheza na moto

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un

Marekani imeionya serikali ya Korea kaskazini kuacha mpango wake wa kucheza na moto na kuachana na mpango wake wa kurusha kombora ambalo imepanga kulirusha licha ya kuonywa na jamii yakimataifa na kuhofia kuchochea moto katika visiwa vya Peninsula.

Matangazo ya kibiashara

Marekani na Korea Kusini zimeweka majeshi yao kwenye tahadhari leo alhamisi kufuatia vitisho vya Korea Kaskazini na matamshi ya kichochezi ambayo yamekuwa yakitolewa na serikali hiyo ya Korea Kaskazini ambayo pia imeendelea kukaidi wito wa jamii ya kimataifa.

Tangu mwezi Februari mwaka 2012 Pyongyang imefanya majaribio mawili ya makombora ambapo moja pekee la Desemba ndilo lililofaulu, jambo lililochukuliwa na jamii ya kimataifa kama jaribio la makombora ya Nyuklia na kutiliwa vikwazo na Umoja wa Mataifa.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuk Hagel amesema Korea Kakszini incheza na moto na haina nia ya kutafuta muafaka kwa hali ambayo ilikutwa tete, na ambapo amesema Serikali ya Marekani ipo tayari kwa lolote, na itajibu uchochezi wa aina yoyore kutoka kwa Korea Kaskazini.

Serikali ya Pyongyang imeweka makombora yake mawili ya Musudan, yenye umbali wa kilometa elfu nne na ambayo yaweza kufika hadi korea Kusini, Japan na kisiwa cha Marekani cha Guam ambako majarabio ya kijeshi yamefanyika kujiandaa iwapo Korea ya Kaskazini itatekeleza hatuwa yake hiyo ya kurusha makombora.