Umoja wa mataifa-Afrika ya kati-Congo DR

Anthonio Guterres akutana na wakimbizi wa Afrika ya kati waliokimbilia Congo DR

Kamishna mkuu wa Uomoja wa mataifa UN anayeshughulikia wakimbizi,Anthonio Guterres
Kamishna mkuu wa Uomoja wa mataifa UN anayeshughulikia wakimbizi,Anthonio Guterres Reuters

Kamishna mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya wakimbizi Antonio Guterres,amekutana na baadhi ya maelfu ya raia wa afrika ya kati waliokimbilia Jamuhuri ya demokrasia ya Congo baada ya waasi kupindua serikali ya raisi Francois Bozize.

Matangazo ya kibiashara

Guterres alifanya ziara huko Zongo na mji mwingine wa jirani miji ambayo yote inapatikana nchini DRC maeneo ya mto Ubangi kutokea mji mkuu wa wa Afrika ya kati Bangui mji ambao waasi wa seleka waliutia mikononi mwao mwezi uliopita.

Takribani raia elfu nne,wa Afrika ya kati wanaishi katika makambi katika miji miwili huku wengine wakikadiriwa kufikia elfu tatu walivuka mpaka kuwakimbia seleka.

Guterres amesema kuwa amefanya ziara makusudi ili kuleta unafuu kwa wakimbizi hao ambao wamekumbwa na mgogoro uliosahaulika kwa jamuhuri ya watu wa Afrika ya kati kwakuwa ziara hiyo itavutia misaada kutoka kwa wahisani na kuleta mshikamano kwa watu wa DRC ambao wamefungua mioyo na mipaka yao.

Waasi wa Seleka, wakiongozwa na Michel Djotodia, waliutia mikononi mwao mji mkuu wa Bangui mnamo tarehe 24 mwezi march na kuuondoa utawala wa raisi Francois Bozize mbali ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwezi january.