PAKISTAN

Pervez Musharraf afungiwa kuwania uongozi nchini Pakistan

Kiongozi wa zamani wa Pakistan Pervez Musharraf amefungiwa kushiriki kwa namna yeyote ile katika Uchaguzi Mkuu mwezi Mei mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Musharraf ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi nchini humo amefungiwa na tume ya uchaguzi nchini humo hatua ambayo inaamisha kuwa hawezi kuwania wadhifa wowote wa uongozi nchini humo.

Wakili wa Musharraf hata hivyo amesema atakata rufaa kupinga uamuzi wa tume hiyo anaosema haukuwa wa haki.

Musharaf alirudi nyumbani mwezi uliopita kutoka Dubai alikokuwa anaishi, na kusema kuwa amerudi nyumbani ili kuikoa Pakistan.

Kiongozi huyo wa zamani pia anakabiliwa na kesi mbalimali ikiwemo ya uhaini huku, kundi la kigaidi la Taliban ambalo limeendelea kupinga serikali nchini humo ikisema inalenga kumshambulia.

Mussaraf mwenye umri wa miaka 69 alikuwa rais wa kumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 2001 hadi 2008 kabla ya kujiuzulu na kukimbilia ukimbozini jijini London nchini Uingereza.

Wakati tangazo hilo likitolewa, watu wanne wameuawa baada ya msafara wa upinzani wa chama cha PML-N kuvamiwa Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.