MAREKANI

Mshukiwa wa mashambulizi ya mabomu ya Boston aonekana kwenye kanda ya Video

Maafisa wa Ujajusi wa FBI wanaochunguza mashambulizi ya mabomu yaliyotokea mjini Boston nchini Marekani wakati wa mashindano ya mbio ndefu siku ya Jumatatu wanasema wamepata picha ya mshukiwa aliyetekeleza mashambuzli hayo.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa baraza la jiji la Boston Stephen Murphy amesema kuwa kanda ya video ilimnasa mtu akiweka mfuko katika eneo la mstari wa mwisho wa kumalizia mbio hizo na kuondoka.

Awali, maafisa wa FBI walikanusha ripoti kuwa tayari walikuwa wamemkata mshukiwa wa tukio hilo kama ilivyokuwa imeripotiwa hapo awali na vyombo mbalimbali vya habari.

Watu watatu waliopoteza maisha yao baada ya mashambulizi hayo mawili na zaidi ya 170 kujeruhiwa.

Rais Barrack Obama antarajiwa kuzuru mji wa Boston siku ya Alhamisi kuhudhuria ibada ya wafu na kutoa pole kwa walioathiriwa na tukio hilo.

Obama amesema kuwa lazima waliotekeleza mashambulizi hayo wachukuliwe hatua za kisheria, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akilaani tukio hilo.

Miaka kumi iliyopita mashambulizi ya mabomu yalisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tatu  mjini New York,Washington DC  na Pennsylvania.