Sudani

Kiongozi wa Waasi wa Darfur nchini Sudan auawa

Rais wa Sudani Omar Hassan Al Bashir,anayetafutwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC
Rais wa Sudani Omar Hassan Al Bashir,anayetafutwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC

Kiongozi wa Waasi katika Jimbo la Darfur,nchini Sudan Saleh Jerbo aliyeshtakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC ameuawa mjini humo, Waasi na kikosi chake cha ulinzi wameeleza. 

Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema kuwa Jerbo aliuawa kaskazini mwa Darfur tarehe 19 mwezi huu na kuzikwa siku hiyo hiyo.
 

Jerbo na Kiongozi mwenzake Abdallah Banda, wanakabiliwa na makosa matatu ya uhalifu wa kivita kwa kuongoza mashambulizi dhidi ya Walinda amani wa Umoja wa Afrika kaskazini mwa Darfur yaliyofanyika mwezi Septemba mwaka 2007 na kusababisha watu 12 kupoteza maisha.
 

Wawili hao walikuwa wanatarajiwa kufika Mahakama ya The Hague kuyakabili mashtaka yao ifikapo mwezi Mei mwaka 2014.
 

Washukiwa hao walijisalimisha mbele ya Mahakama ya ICC mwezi June mwaka 2010 na kutoa wito kwa wengine wanaoshukiwa kujisalimisha Mahakamani hapo.
 

Waasi wengine wanne wanatafutwa wakishutumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kivita mjini Darfur akiwemo Rais wa Sudan Omar al Bashir.
 

Takriban watu 300,000 wameuawa jimboni Darfur na Watu milioni mbili wameyakimbia makazi yao huku Serikali ya Sudan ikisema watu 10,000 wamepoteza maisha.