Bangladeshi

Polisi nchini Bangladeshi wadhibiti maandamano ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo

Vikosi vya uokoaji vikiendelea na zoezi ya kuwapata Watu waliofunikwa na Vifusi
Vikosi vya uokoaji vikiendelea na zoezi ya kuwapata Watu waliofunikwa na Vifusi REUTERS/Andrew Biraj

Polisi nchini Bangadeshi imefanya kazi ya kudhibiti makundi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Nguo ambao wamefanya maandamano makubwa kufuatia vifo vya wenzao Takriban 300 vilivyosababishwa na kuporomoka kwa Jengo lililokuwa na viwanda vya nguo.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yamekuja wakati huu ambapo jitihada za uokoaji zikiingia siku ya tatu hii leo.
 

Ajali ya kuporomoka kwa jengo mjini Dhaka limezua shutma kuwa makampuni ya nguo ya nchi za magharibi yaliyo nchini Bangladeshi yanaweka mbele maslahi yao kuliko usalama wa mahali pa kazi na Wafanyakazi.
 

Shughuli za uokoaji jana usiku zilionesha kuzaa matunda baada ya miili 45 kupatikana na kutoa matumaini kwa Watu waliokuwa wakisubiri katika eneo la ajali wakiwa na tumaini la kuwapata wapendwa wao huku kukiwa na taarifa kua miili mingine ingali imefunikwa na vifusi.
 

Zaidi ya watu 2,300 wameokolewa wakiwa hai tangu siku ya jumatano.
 

Takriban viwanda 4,500 vimefungwa kufuatia maandamano na kwa kuhofia uharibifu wa mali,siku ya jumamosi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko huku vyama vya Wafanyakazi vikiitisha mgomo siku ya jumapili kudai mazingira mazuri ya kufanya kazi.
 

Ghadhabu ya Wafanyakazi hao imepamba moto baada ya kubainika kuwa Viongozi wa Kiwanda waliwaamuru wafanyakazi kurejea katika jengo hilo,ingawa nyufa za jengo hilo zilikwishaonekana tangu siku ya jumanne.
 

Polisi wanaendelea kuwatafuta wamiliki wa Kiwanda na cha nguo na Wamiliki wa jengo baada ya Waziri Mkuu wa Bangladeshi Sheikh Hasina kuapa kuwafikisha Watu hao mbele ya Sheria.