KENYA

Uchunguzi juu ya kifo cha Seneta wa Makueni Kenya,Mutula Kilonzo waanza.

Seneta wa Makueni kaskazini mashariki mwa Kenya,Mutula Kiolonzo amefariki dunia ghafla jumamosi.
Seneta wa Makueni kaskazini mashariki mwa Kenya,Mutula Kiolonzo amefariki dunia ghafla jumamosi. starfm.co.ke

Jeshi la polisi nchini Kenya kwa sasa linachunguza kuhusiana na kifo cha ghafla cha seneta wa eneo la Makueni kaskazini mashariki mwa Kenya Mutula Kilonzo, aliyefariki jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Seneta huyo alibainika ameaga dunia akiwa nyumbani kwake saa saba mchana siku ya jumamosi baada ya wafanyakazi wake kuvunja mlango na kuukuta mwili wa Seneta huyo.

Kifo cha ghafla cha kiongozi huyo kimeshangaza raia wengi nchini Kenya ambapo seneta wa Machakos Johnston Mudhama amesema kuwa uchunguzi tayari umeanza kwa kumuita daktari wa familia kuanza uchunguzi haraka.

Katika hatua nyingine Seneta Mudhama amewataka wakenya kuwa watulivu kwani uchunguzi utabaini kilichokatisha uhai wa Mutula Kilonzo kwa ghafla na taarifa itatolewa.

Seneta Mutula Kilonzo mwenye umri wa miaka 64 aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya uwaziri wa elimu katika serikali ya raisi Mwai Kibaki.