SYRIA

Waziri mkuu wa Syria anusurika kuuawa kwa bomu mjini Damascus

RFI

Waziri Mkuu wa Syria Wael al-Halqi hii leo amenusurika kuuawa baada shambulio la bomu lililokuwa limelenga msafara wake katikati ya mji wa Damascus nchini humo.Taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa imeeleza kuwa pamoja na shambulio hilo la kigaidi, waziri mkuu huyo dakta Wael al-Halqi hajajeruhiwa na yuko salama. 

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo watu wasiopungua sita wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa kutokana na shambulio hilo huku magari kadhaa yakiharibiwa vibaya katika eneo la tukio.
 

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa shambulio hilo lilikua pigo kubwa kwa serikali ya Bashar Al Assad kama lingefanikiwa kumuua waziri mkuu huyo.
 

Katika siku za hivi karibuni majeshi ya serikali yameonekana kupata nguvu katika uwanja wa vita na shambulio hilo limefanywa na waasi ili kutoa ujumbe kwa serikali kuwa bado waasi wana nguvu.