SYRIA-UN

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Syria isizuie uchunguzi wa silaha za kemikali

RFI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Ban Ki Moon ametoa wito kwa Damascus kutowekea vikwazo uchunguzi wa kimataifa juu ya tuhuma kuwa Serikali ya Syria imekuwa ikitumia Silaha za Kemikali.  

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amekutana na mkuu wa timu ya UN ya uchunguzi Ake Sellstrom na kusema kuwa ataichukua ripoti yake kwa umakini mkubwa.

Amesema kuanzia sasa serikali ya Syria haipaswi kuchelewesha uchunguzi na kuacha kuweka masharti yoyote ambayo yatakwamisha uchunguzi huo na kuuacha uendelee.

Wakati wito huo ukitolewa waziri Mkuu wa Syria Wael al -Haqi hiyo jana amenusurika kuuawa baada ya Msafara wake kukoswa koswa na Bomu jijini Damascus, ikiwa ni moja ya mashambulizi dhidi ya Washirika wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Al Assad.
 

Shambulio lilifuatiwa na shambulizi jingine la anga katika mji anaoishi Waziri huyo, Jassem, katika jimbo la Daraa, shambulio lililogharimu maisha ya Watu 11 wakiwemo Waasi wanane.