Uholanzi

Uholanzi yapata mfalme mpya, ni baada ya Malkia Beatrix kumwachia mtoto wake

Mfalme mpya wa UHOLANZI Willem-Alexander
Mfalme mpya wa UHOLANZI Willem-Alexander Reuters

Wananchi wa uholanzi hii leo wanashuhudia kusimikwa rasmi kwa mwana mfalme wa Malikia Beatrix, Willem-Alexander kama mfalme mpya wa taifa hilo katika sherehe za kihistoria. 

Matangazo ya kibiashara

Willem-Alexander anakuwa mfalme wa kwanza kijana kuongoza taifa la Uholanzi katika sherehe ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dunia.

Siku ya jumatatu malkia Beatrix alitangaza rasmi kukabidhi madaraka ya kifalme kwa mtoto wake wa kiume, Alexander katika tukio lililoshuhudiwa nchi nzima kupitia njia ya televisheni.

Maelfu ya wananchi toka sehemu mbalimbali za nchi na dunia wamekusanyika kwenye uwanja wa Dam kushuhudia tukio hili la kihistoria ambalo halijawahi kushuhudiwa kwenye mataifa yanayoongozwa kifalme ambapo rangi za chungwa zimepamba mji wa Amsterdam.

Mfalme Willem-Alexander mwenye umri wa miaka 46 amemuoa Maxima Zorreguieta mzaliwa wa Argentina mwenye umri wa miaka 41 ambaye sasa atafahamika kama malikia Maxima.tional anthem.